Pata taarifa kuu
SOKA-MICHEZO

Soka: Ujerumani, taifa la kwanza kufuzu Kombe la Dunia 2022

Jumatatu, Oktoba 11, Ujerumani ilikuwa timu ya kwanza kukata tiketi yake ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia 2022 huko Qatar baada ya kushinda 4-0 huko North Macedonia. Huu ni ushindi wake wa 18 mfululizo tangu mwaka 1954 kwa awamu ya mwisho ya Kombe la Dunia.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani baada ya ushindi wao wa 4-0 dhidi ya North Macedonia, Oktoba 11, 2021 huko Skopje.
Wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani baada ya ushindi wao wa 4-0 dhidi ya North Macedonia, Oktoba 11, 2021 huko Skopje. Robert ATANASOVSKI AFP
Matangazo ya kibiashara

Bingwa wa Dunia mnamo mwaka 2014 nchini Brazil, Ujerumani ni taifa la kwanza kujikatia tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka 2022. Ujerumani imefuzu kwa mara ya 18 mfululizo tangu 1954 kwa awamu ya mwisho ya Kombe la Dunia. Kwa Kombe la Dunia la 2018 nchini Urusi, Wajerumani walijikatia tiketi yao bila usumbufu wowote. Isipokuwa kwamba walikuwa wameondolewa katika hatua ya makundi katika nchi ya Dostoevsky.

Bado kazi kidogo ya kufanya

Na alama 8 mbele ya Romania, wakati huo huo ikishinda Armenia 1-0, mabingwa wa dunia mara nne hawawezi kufikiwa tena. Timu pekee iliyofuzu hadi sasa ni Qatar, nchi mwenyeji. Tangu kuteuliwa kwa Hansi Flick kama meneja kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani, ambaye alichukua nafasi ya Joachim Löw baada ya michuano ya Euro msimu wa joto uliopita, Ujerumani imeshinda mara 5 kati ya mechi 5 na ilifunga mabao 18 na kufungwa bao 1 pekee.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.