Pata taarifa kuu
TOTTENHAM-SOKA

Uingereza: Harry Kane atangaza kwenye Twitter kwamba anabaki Tottenham

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane alitangaza kwenye akaunti yake ya Twitter siku ya Jumatano kwamba hataondoka Tottenham msimu huu wa joto, kwani Manchester City ilijaribu kumsajili na inaonekana kuwa inajaribu kutoa kitita kikubwa cha fedha kwa kumpata mchezaji huyo.

Mshambuliaji wa England Harry Kane kutoka Tottenham wakati wa mapokezi ya Aston Villa kwenye Ligi Kuu mnamo Mei 19, 2021
Mshambuliaji wa England Harry Kane kutoka Tottenham wakati wa mapokezi ya Aston Villa kwenye Ligi Kuu mnamo Mei 19, 2021 DANIEL LEAL-OLIVAS POOL/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

"Nitakabaki Tottenham msimu huu wa joto na nitajitahuidi kwa vyovyote vile kusaidia timu iweze kufaya vizuri," mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza aliandika, na hivyo kusitisha uvumi uliyokuwa ukisambaa.

Akiwa bado yuko chini ya mkataba na Spurs hadi 2024, Kane 28, alikuwa ametangaza kuondoka katika klabu yake aliojiunga nayo mnamo 2004.

Manchester City, ikitafuta mshambuliaji wa kati baada ya kuondoka kwa Sergio Agüero (FC Barcelona) baada ya mkataba wake kutamatika msimu huu wa joto, ilikuwa imependekeza kitita cha pauni Milioni 100 (sawa na Milioni 117 za Euro) ambazo zilikataliwa na mwenyekiti wa Tottenham, Rais Daniel Levy , mashuhuri kwa ushupavu wake katika mazungumzo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.