Pata taarifa kuu
COPA AMERICA

Argentina yaishinda Colombia kufuzu fainali ya Copa America

Emiliano Martinez, kipa wa timu ya taifa ya Argentina amekuwa shujaa, baada ya kuisaidia nchi yake kufuzu katika hatua ya fainali kuwania taji la soka, la Copa America huko Kusini mwa Afrika.

Kipa wa Argentina  Emiliano Martinez  akiokoa penalti katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Colombia Julai 07 2021
Kipa wa Argentina Emiliano Martinez akiokoa penalti katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Colombia Julai 07 2021 EVARISTO SA AFP
Matangazo ya kibiashara

Argentina imefuzu baada ya kuifunga Colombia mabao 3-2 kupitia mikwaju ya penalti, katika mchuano wa nusu fainali uliochezwa mjini Brasilia.

Lautaro Martinez aliipa Argertina bao la ufunguzi katika dakika ya 7 ya mchuano huo, kabla ya Luis Fernando Díaz Marulanda kuisawazishia Colombia katika dakika ya 61 ya mchuano huo.

Argentina sasa itachuana na Brazil katika mechi ya fainali ikayopigiwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro.

Miaka miwili iliyopita, Brazil ilicheza na Argentina katika hatua ya nusu fainali na kushinda taji hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.