Pata taarifa kuu
JAPANI-CORONA-MICHEZO

Uchunguzi: Nusu ya wakazi wa Tokyo wapinga michezo ya Olimpiki ya 2021

Karibu zaidi ya nusu ya wakaazi wa Tokyo wanapinga michezo ya Olimpiki iliyokuwa imepangwa kupigwa mwaka 2020 na baadae kuahirishwa hadi mwaka 2021 katika jiji lao kwa sababu ya janga la Corona.

Makubaliano ya tarehe mpya yamefikiwa wakati wa mkutano kwa njia ya simu yaloiyofanywa kati ya Rais wa IOC Thomas Bach, Rais wa Tokyo 2020 Mori Yoshirō, Gavana wa Tokyo Koike Yuriko na Waziri wa Olimpiki na Paralimpiki Hashimoto Seiko.
Makubaliano ya tarehe mpya yamefikiwa wakati wa mkutano kwa njia ya simu yaloiyofanywa kati ya Rais wa IOC Thomas Bach, Rais wa Tokyo 2020 Mori Yoshirō, Gavana wa Tokyo Koike Yuriko na Waziri wa Olimpiki na Paralimpiki Hashimoto Seiko. REUTERS/Issei Kato
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo uliendeshwa na shirika la habari la Japan la Kyodo na kituo cha television cha Tokyo MX na kuchapishwa leo Jumatatu, Juni 29.

Mwezi Machi mwaka huu, Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki IOC na Kamati ya kimataifa ya Paralimpiki IPC au Olimpiki ya watu wenye ulemavu, kwa pamoja na kamati ya maandalizi ya Tokyo 2020, Serikali ya mji wa Tokyo na serikali ya Japani walitangaza kuwa kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona, COVID-19, sasa michezo ya Olimpiki iliyokuwa ifanyike mwaka huu mjini Tokyo, itafanyika mwaka ujao wa 2021.

Mamlaka hizo zimetangaza kuwa michezo ya Olimpiki itafanyika kuanzia tarehe 23 Julai hadi tarehe 8 Agosti mwakani, wakati ile ya watu wenye ulemavu ikifanyika kuanzia tarehe 24 Agosti hadi Septemba mwaka huo wa kesho 2021.

Makubaliano ya tarehe mpya yamefikiwa wakati wa mkutano kwa njia ya simu yaloiyofanywa kati ya Rais wa IOC Thomas Bach, rais wa Tokyo 2020 Mori Yoshirō, Gavana wa Tokyo Koike Yuriko na Waziri wa Olimpiki na Paralimpiki Hashimoto Seiko.

Tarehe mpya ni mwaka mmoja kamili tangu tarehe ambazo zilikuwa zimepangwa kufanyika kwa michezo ya Olimpiki ya mwaka huu 2020.

Taarifa ya awali ya OIC imesema kuwa wanamichezo wote ambao tayari walikuwa wamefuzu na tayari wamepangiwa kushiriki katika michezo ya Olimpiki yam waka 2020 watasalia kama walivyo bila kubadilishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.