Pata taarifa kuu
KENYA-CECAFA-UGANDA-SOKA

Zedekiah ‘Zico’ Otieno kuiongoza Harambee Stars katika mechi mbili za CECAFA

Naibu kocha wa timu ya taifa ya Kenya, Zedekiah ‘Zico’ Otieno ataingoza Harambee Stars katika mchuano wake wa pili wa kundi B, kutafuta taji la CECAFA dhidi ya Sudan.

Wachezaji wa Kenya Harambee Stars watacheza na Sudan, Dese,ba 10 2019
Wachezaji wa Kenya Harambee Stars watacheza na Sudan, Dese,ba 10 2019 Football Kenya Limited
Matangazo ya kibiashara

Mechi hiyo itachezwa Jumanne jioni katika uwanja wa KCCA jijini Kampala nchini Uganda.

Hatua hii imekuja, baada ya waandalizi wa michuano ya CECAFA, kumfungia mechI mbili kocha mkuu Francis Kimanzi kutofika uwanjani baada ya kupatikana na kosa lisilokuwa la kimichezo, wakati Kenya ilipokuwa inacheza na Tanzania.

Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye katika barua aliyomwandikia kiongozi wa ujumbe wa Kenya, amesema Kimanzi alipatikana na kosa la kumsumbua mwamuzi wa nne na kumfukuza kutoka katika chumba cha wachezaji kupumzika na kuwafungia ndani kwa dakika 10, suala ambalo lilichelewesha kuanza kwa mechi hiyo.

Mechi ya kwanza, Kenya ambao ni mabingwa watetezi wa taji hili, walianza vema kwa kuifunga Tanzania bao 1-0 na iwapo wataifunga Sudan, watakuwa wamefuzu katika hatua ya nusu fainali.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.