Pata taarifa kuu
KOMBE LIGI YA MATAIFA ULAYA

Ureno yatwaa taji la ligi ya matiafa ya Ulaya, taji la 2 katika miaka 3

Timu ya taifa ya Ureno imefanikiwa kutwaa taji lake la pili kubwa katika kipindi cha miaka mitatu baada ya kuifunga Uholanzi katika mchezo wa fainali wa ligi ya mataifa ya Ulaya.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Ureno wakishangilia ushindi katika mchezo wa fainali dhidi ya Uholanzi.
Wachezaji wa timu ya taifa ya Ureno wakishangilia ushindi katika mchezo wa fainali dhidi ya Uholanzi. Carl Recine/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kikosi cha kocha Fernando Santos kilifanikiwa pia kutwaa taji la mataifa ya Ulaya mwaka 2016, ambapo goli la Goncalo Guedes katika kipindi cha pili lilitosha kuipa Ureno ushindi wa bao 1-0 mjini Porto.

Guedes anayekipiga na klabu ya Valencia ya Uhispania, alifunga kwa kupiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Uholanzi Jasper Cillessen.

Uholanzi ilijaribu kufanya kila linalowezekana kurejesha bao hilo, ambapo kichwa cha mshambuliaji wake Memphis Depay kiliokolewa na kipa wa Ureno Rui Patricio ambaye aliokoa mchomo mwingine wa Marten de Roon.

Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin akimpigia makofi mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo akiwa amebeba kombe
Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin akimpigia makofi mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo akiwa amebeba kombe Carl Recine/Reuters

Timu ya taifa ya Uingereza ilimaliza katika nafasi ya tatu baada ya kupata ushindi kwa njia ya matuta dhidi ya Uswis.

Mshambuliaji wa Ureno ambaye pia ni nahodha, alifunga magoli 3 katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Uswis lakini akashindwa kufikisha bao la 88 la kimataifa dhidi ya Uholanzi.

Ronaldo alimanusura aifungue bao timu yake katika kipindi cha kwanza na cha pili lakini shuti lake liliokolewa na kipa wa Barcelona Cillessen huku mara kadhaa akipaisha mashuti yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.