Pata taarifa kuu
UGANDA-TANZANIA-SOKA

Uganda yajiandaa kumenyana na Tanzania

Timu ya taifa ya soka ya Uganda, ipo nchini Misri kwa maandalizi ya mchuano wa mwisho wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika dhidi ya Tanzania, siku ya Jumapili.

Dennis Onyango, nahodha wa timu ya taifa ya Uganda.
Dennis Onyango, nahodha wa timu ya taifa ya Uganda. Denis Onyango/Twitter.com
Matangazo ya kibiashara

Mechi hiyo itachezwa jijini Dar es Salaam, na Uganda wanakwenda katika mechi hiyo wakiwa tayari wamefzu katika michuano hiyo itakayofanyika nchini mwezi Juni, lakini kazi kubwa inasalia kwa Tanzania inayohitaji ushindi.

Kocha wa Uganda, Sebastian Desabre, amesema wanataka kumaliza vema kampeni yao na hivyo wanahitaji kushinda ili kupata alama tatu muhimu.

Miongoni mwa wachezaji walio kambini nchini Misri ni Nahodha Dennis Onyango, Khalid Aucho, Emmanuel Okwi miongoni mwa wengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.