Pata taarifa kuu
CAF-MISRI-AFCON 2019-SOKA

Michuano ya AFCON 2019 kuchezwa Misri

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2019 AFCON itapigwa nchini Misri, kuanzia Juni 15 hadi Julai 13, bodi ya uongozi ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) imeamua leo Jumanne Januari 8 mjini Dakar.

Rais wa CAF, Ahmad Ahmed.
Rais wa CAF, Ahmad Ahmed. CRISTINA ALDEHUELA / AFP
Matangazo ya kibiashara

CAF imeamua kuteuwa Misri badala ya Afrika Kusini. Awali Cameroon ilitarajiwa kuwa mwenyeji wa michuano hii ya AFCON 2019, ambayo itajumuisha timu kwa mara ya kwanza timu 24 badala ya 16.

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika itapigwa kwa mara ya tano katika historia yake katika ardhi ya Misri, baada ya mwaka 1959, 1974, 1986 na 2006. Uamuzi huu umechukuliwa na bodi ya uongozi ya Shirikisho la Soka la Afrika (ComEX), iliyokutana tarehe 8 Januari 2019 katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.

ComEx imeteua Misri kama mwenyeji wa michuano ya AFCON 2019 badala ya Afrika Kusini, nchi nyingine iliwania kuchukua nafasi ya Cameroon.

Hata hivyo hali ya usalama nchini Misri bado suala linaloendelea kujadiliwa na viongozi wa CAF.

Lakini viongozi wa Misri wamesema suala hilo litapatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.