Pata taarifa kuu
MISRI-LIVERPOOL-MOHAMMED SALAH

Mohammed Salah aweka rekodi ya mabao Liverpool

Nyota wa soka wa kimataifa wa Misri Mohammed Salah ameweka rekodi ya mapema kufunga mabao 50 katika klabu ya Liverpool ya Uingereza. 

Mohammed Salah akishnagilia na wachezaji wenzake wa Liverpool
Mohammed Salah akishnagilia na wachezaji wenzake wa Liverpool Andrew Yates/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mshindi huyo wa goli bora katika tuzo za mwaka jana aliweka rekodi hiyo jana alipoiongoza Liverpool kuishinda Crvena Zvezda katika mchezo wa Ligi ya mabingwa Ulaya.

Sasa Mohammed Salah amefikisha mabao 50 katika mechi 65 alizoichezea Liverpool tangu ajiunge nayo mwaka 2017 kwa dau la paundi Milioni 40 akitokea AS Roma ya Italia.

Kocha wa Liverpool amemsifu Salah na kuongeza kuwa ni mchezaji wa kuchungwa zaidi barani Ulaya.

Liverpool imefunga mabao 48 katika ligi ya mabingwa Ulaya, ikiizidi Real Madrid ambayo imefunga mabao 38.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.