Pata taarifa kuu
CAF-KLABU BINGWA-AL AHLY- ESPERANCE DE TUNIS

Al Ahly kumenyana na Esperance de Tunis fainali ya klabu bingwa Afrika

Al Ahly ya Misri, itacheza na Esperance de Tunis, ya Tunisia, katika fainali ya kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika, itakayofanyika mwezi Novemba.

Klabu ya Al Ahly, ikimenyana na  Entente Setif  katika mechi ya nusu fainali Oktoba 23 2018
Klabu ya Al Ahly, ikimenyana na Entente Setif katika mechi ya nusu fainali Oktoba 23 2018 www.cafonline.com
Matangazo ya kibiashara

Licha ya kufungwa mabao 2-1 na Entente Setif ya Algeria siku ya Jumanne usiku, ilifuzu kwa jumla ya mabao 3-2 kwa sababu ya ushindi wa nyumbani wa mabao 2-0 zaidi ya wiki tatu zilizopita.

Hii ilikuwa ni mechi ya kwanza kati ya nane zilizopita kwa ya Al Ahly inayofunzwa na kocha Mfaransa Patrice Carteron, kupoteza.

Mabingwa hao mara nane wa taji hili, wataanza kuwa wenyeji wa mchuano wa fainali tarehe mbili mwezi Novemba jijini Cairo, kabla ya mechi ya mwisho kuchezwa mjini Rades, tarehe 9.

Esperance de Tunis, nayo ilifuzu  baada ya kupata ushindi wa mbao 3-4. Licha ya kufungwa ngenini na Primero de Agosto bao 1-0, ikicheza nyumbani ilifanikiwa kupata ushindi wa manao 4-2.

Mshindi baada ya mechi hizo mbili, atajinyakulia Dola za Marekani Milioni 2.5 na kufuzu kucheza kombe la dunia, baina ya vlabu katika nchi ya Falme za Kiarabu mwezi Desemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.