Pata taarifa kuu
KIKAPU-TANZANIA-KENYA-MISRI-FIBA

Michuano ya kanda ya tano Afrika kufikia tamati Oktoba 7, Jijini Dar es Salaam.

Michuano ya mpira wa kikapu kanda ya tano Afrika inaendelea kurindima Jijini Dar es Salaam nchini Tanzania ikishirikisha timu kutoka mataifa tisa. 

Oilers ilipopambana na timu kutoka Rwanda katika Uwanja wa ndani wa Taifa Jijini Dar es Salaam Oktoba 5, 2018
Oilers ilipopambana na timu kutoka Rwanda katika Uwanja wa ndani wa Taifa Jijini Dar es Salaam Oktoba 5, 2018 RFI Kiswahili/Fredrick Nwaka
Matangazo ya kibiashara

Michuano hiyo itafikia kilele chake Oktoba 10 na Tanzania ikiwakilishwa na timu tatu ambazo ni Oilers na JKT ambayo imetoa timu mbili JKT wanawake na JKT wanaume.

Hata hivyo timu za Tanzania hazijaanza vizuri michuano hiyo na kujikuta zikifanya vibaya ikilinganishwa na wawakilishi kutoka mataifa mengine.

Changamoto ya maandalizi hafifu na ukosefu wa fedha imesababisha wawakilishi wa Tanzania kutofanya vizuri kwenye michuano hiyo.

Kenya inawakilishwa na timu ya Bandari na KPA.

Mwandishi wa habari za Michezo kutoka nchini Kenya Lenat Matheka anasema timu za Afrika Mashariki zinashindwa kufua dafu kutokana na kutokuwa na maandalizi mazuri ikilinganishwa na timu kutoka Misri.

Endelea kufuatilia mtandao wetu kufahamu zaidi kuhusu michuano hii ambayo Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania ni mwenyeji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.