Pata taarifa kuu
SOKA-YANGASC-TANZANIA

Yanga yawarejesha kundini Mrisho Ngassa na Deus Kaseke

Klabu ya Yanga ya Tanzania imewasajili wachezaji Deus Kaseke na Mrisho Ngassa kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Deus Kaseke (kulia) na Mrisho Ngassa (kushoto) wakitambulishwa na mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Yanga, Hussein Nyika
Deus Kaseke (kulia) na Mrisho Ngassa (kushoto) wakitambulishwa na mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Yanga, Hussein Nyika www.yangasc.co.tz
Matangazo ya kibiashara

Wachezaji hao wametambulishwa leo katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Jangwani na Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika.

Wachezaji wote waliwahi kuitumikia Yanga kwa misimu tofauti. Deus Kaseke anajiunga na Yanga akitokea Singida United na Kaseke anatokea Singida United.

Wachezaji wengine waliosajiliwa na Yanga ni Mohammed Issa kutoka Mtibwa Sugar na Jafar Mohammed kutoka Majimaji ya Songea.

Yanga ni wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Afrika ambapo wanashiriki hatua ya makundi ya taji la shirikisho.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.