Pata taarifa kuu
MISRI-SOKA-KOMBE LA DUNIA

Misri kuachana na kocha Hector Cuper

Shirikisho la soka nchini Misri, EFA limesema halitampa mkataba mpya kocha Hector Cuper raia wa Argentina, baada ya matokea mabaya katika michuano ya kombe la dunia, inayoendelea nchini Urusi.

Kocha wa timu ya taifa ya Misri Hector Cuper
Kocha wa timu ya taifa ya Misri Hector Cuper Pierre René-Worms / RFI
Matangazo ya kibiashara

Misri iliondolewa mapema katika michuano hiyo mikubwa duniani baada ya kufungwa mechi zake zote dhidi ya Uruguay, Urusi na Saudi Arabia katika kundi A.

Cuper, amekuwa akiiifunza Misri tangu mwaka 2015, na aliisaidia nchi hiyo kufuzu katika michuano ya kombe la dunia na fainali ya mataifa bingwa barani Afrika AFCON nchini Gabon.

Baadhi ya mashabiki wa soka nchini Misri, wamekuwa wakimkosoa namna alivyopanga kikosi chake wakati wa michuano ya kombe la dunia na kulaumiwa kwa kuwaacha nje wachezaji muhimu.

Katika mechi 38 alizowahi kuiongoza Misri, tangu mwaka 2015, alifanikiwa kupata ushindi mara 20 na kupoteza mechi 12 huku Misri ikitoka sare mara sita chini ya uangalizi wake.

Aidha, Misri walifanikiwa kufunga mabao 53 na kufungwa mabao 31 chini ya kocha Cuper.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.