Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-MICHEZO-USALAMA

Michezo ya Jumuiya ya Madola: Wanariadha 200 waomba hifadhi ya ukimbizi

Baada ya mashindano ya Michezo ya Jumuiya ya Madola, wanariadha karibu 200 wameomba hifadhi ya ukimbizi nchini Australia. Watu karibu 200 wameomba hifadhi ya ukimbizi nchini Australia baada ya kusafiri katika nchi hiyo kwa ajili ya Michezo ya Jumuiya ya Madola mwezi uliopita.

Baadhi ya wanariadhaa walioshiriki katika michezo ya Michezo ya Madola nchini Australia wametoweka.
Baadhi ya wanariadhaa walioshiriki katika michezo ya Michezo ya Madola nchini Australia wametoweka. AAP/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hadi sasa, maombi 190 yameorodheshwa, wakati ambapo wanariadha wengine 15 au maafisa engine wa mafunzo wameomba aina nyingine za visa.

Malisa Golightly, afisa wa Idara ya Mambo ya Ndani amethibitisha "ombi hilo la ukimbizi linalojumuisha watu wengi" wakati wa kikao cha bunge katika mji mkuu wa Australia, Canberra.

Karibu wanariadha 50 bado wanakosekana, Bi Golightly ameongeza.

Idara ya Mambo ya Ndani inafanya kazi kwa minajili ya watu hao wanaoomba hifadhi ya ukimbizi ili kujua nchi wanakotoka.

Ingawa haijulikani nchi wanakotoka wanariadha hawa, tayari imearipotiwa kuwa baadhi yao ni kutoka Cameroon, Uganda, Rwanda na Sierra Leone.

Watetezi wa haki za wakimbizi nchini Australia wamesema wanariadha wengi wa Afrika walionekanai baada ya muda wa visa (siku 15) kumalizika Mei 15.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.