Pata taarifa kuu
UGANDA-SOKA

Kocha Micho aachana na Uganda Cranes

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Uganda, Mserbia Milutin “Micho” Sredojevic amesitisha mkataba wa kuendelea kuifunza Uganda.

Kocha Milutin Sredojevic
Kocha Milutin Sredojevic AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya kutoelewana na viongozi wa Shirikisho la soka nchini humo FUFA kuhusu masuala mbalimbali.

Ripoti zinasema kuwa, hatua hii imekuja baada ya kocha huyo kutolipwa mshahara wake kwa miezi kadhaa.

Micho alijiunga na Uganda Cranes mwaka 2013.

Hadi kuondoka nchini humo, aliisaidia Uganda kufuzu katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39.

Uganda Cranes ilifuzu katika fainali ya mataifa bingwa iliyofanyika nchini Gabon mwezi Januari.

Ameondoka baada ya kuiongoza Uganda kufuzu katika hatua ya tatu kufuzu katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani CHAN mwaka ujao nchini Kenya.

Katika mechi 91, alizoongoza akiwa kocha wa Uganda, alishinda mechi 51, kutoka sare 29 na kupoteza mechi 11.

Kumekuwa na ripoti kuwa, huenda Micho mwenye umri wa miaka 47, anakwenda kuifunza klabu ya Orlando Pirates nchini Afrika Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.