Jukwaa la Michezo
Mashindano ya riadha ya dunia kwa vijana yamalizika nchini Kenya
Imechapishwa:
Cheza - 23:31
Kenya imefanikiwa kuandaa mashindano ya dunia ya riadha kwa vijana wasiozidi miaka 18.Mashindano haya yamekuwa yakifanyika kwa muda wa siku tano zilizopita katika uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani jijini Nairobi. Afrika Kusini ilimaliza ya kwanza kwa medali 11, ikifutawa na China pia kwa medali 11. Cuba ilimaliza ya tatu huku Kenya ikimaliza ya nne kwa medali nyingi ambazo ni 15 lakini ikapata medali 4 ya dhahabu.Tunachambua mashindano haya.