Pata taarifa kuu
MPIRA WA MIGUU-CAMEROON

Rigobert Song atolewa chumba cha wagonjwa mahututi, aanza kupumua mwenyewe

Beki wa kati na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon, Rigobert Song ambaye mwishoni mwa juma lililopita alikimbizwa hospitalini akiwa kwenye hali mbaya baada ya kuanguka ghafla nyumbani kwake, ameacha kutumia mashine kupumua.

Mchezaji wa zamani wa Cameroon, Rigobert Song.
Mchezaji wa zamani wa Cameroon, Rigobert Song. .linternaute.com
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ndugu wa familia yake, wamesema kuwa Song kwa sasa yuko nchini Ufaransa ambako amepelekwa kwa matibabu zaidi, baada ya awali kulazwa katika hospitali kuu ya mjini Younde.

Song alianguka ghafla akiwa nyumbani kwake na kupoteza fahamu, ambapo alilazimika kukimbizwa hospitalini, na toka wakati huo alikuwa akitumia mashine maalumu za kupumulia.

Familia yake inasema kuwa ndugu yao sasa ametolewa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi na ameacha kutumia mashine za kupumulia.

Wachezaji wengi wa zamani na wa sasa wa Cameroon wameendelea kutuma salamu za pole kwa familia yake wakimuombea apone haraka na kurejea kwenye hali ya kawaida, ambapo madaktari wanaomtibu wamesema hali yake inaendelea kuimarika.

Songo alianza kuichezea timu yake ya taifa mara ya kwanza September 1993 akiwa na umri wa miaka 17, wakati timu yake ilipocheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki na timu ya taifa ya Mexico jijini Los Angeles, Marekani.

Song ameichezea timu yake ya taifa mara 137 na pia aliwahi kuwa beki kwa timu za ligi kuu ya Uingereza kama vile Liverpool na West Ham.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.