Pata taarifa kuu
NFF-NIGERIA

Kocha Siasia alipa wiki 2 shirikisho la mpira Nigeria, NFF, kumlipa fedha anazodai

Aliekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya vijana ya Nigeria chini ya umri wa miaka 23, Samson Siasia, ametoa muda wa wiki mbili kwa shirikisho la mpira nchini humo NFFm kuwa limemlipa madeni yake yote anayolidai shirikisho hilo.

Matangazo ya kibiashara

Siasia amesema kuwa shirikisho hilo analidai mshahara wa miezi mitano, kuanzia mwezi April hadi mwezi Agosti mwaka huu wakati akikinoa kikosi hicho.

Kocha huyo mwenye tajiriba ya aina yake, aliiongoza Nigeria kushinda medali ya shaba wakati wa michezo ya Olimpiki ya Rio, Brazil iliyomalizika mwezi mmoja uliopita.

Ikiwa ni takribani mwezi mmoja na wiki moja tu imepita toka kocha huyo atangaze kubwaga manyanga kukinoa kikosi hicho kwa kile alichosema ni mizengwe ya shirikisho, kocha Siasia, amesema kwa sasa uvumilivu wake umeisha.

“Nimewapa makataa ya wiki mbili kuwa wamenilipa fedha zangu au nitasimama nje ya ofisi za NFF mjini Abija mpaka wanilipe haki yangu,” alisema Siasia wakati azungumza na shirika la utangaza la Uingereza BBC.

“Nimeweka wazi kwenye barua yangu, kuwa wasaidizi wangu pamoja na mimi lazima tulipwe kile ambacho tulistahili kulipwa kwakuwa kutofanya hivyo sio ubinadamu,” alisema Siasia.

“Tukiwa kama vichwa vya familia zetu, tumejitoa sana kwaajili ya taifam lakini NFF inakataa kutulipa, hii ni zaidi ya kutokuwa na utu!”

Hata hivyo afisa mmoja wa shirikisho la NFF, amesema kuwa Siasia na benchi lake lote la ufundi watalipwa fedha zao, na kuongeza kuwa wao kama uongozi wamesikitishwa na matamshi ya kocha huyo, sababu wanajua kwasasa tunatumia mfumo mpya wa kufanya malipo, kwahivyo lazima utaratibu ufuatwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.