Pata taarifa kuu
UEFA 2020

UEFA yazindua nembo mpya ya michuano ya Euro 2020, uwanja wa Wimbley kuchezewa fainali

Rais mpya wa shirikisho la mpira barani Ulaya, UEFA, Aleksander Ceferini, amezindua rasmi nembo mpya itakayotumika kwaajili ya michezo ya kombe la mataifa Ulaya mwaka 2020, wakati wa sherehe zilizofanyika jijini London.

Nembo mpya ya mashindano ya kombe la Ulaya mwaka 2020, iliyozinduliwa jijini London, 21 September, 2016.
Nembo mpya ya mashindano ya kombe la Ulaya mwaka 2020, iliyozinduliwa jijini London, 21 September, 2016. Reuters / Tony O'Brien Livepic
Matangazo ya kibiashara

Nembo hii inaonesha rangi mchanganyiko za mashabiki wakiwa wamesimama kando ya kombe lililopewa jina la Henri Delaunay katika daraja la kijani, ikiwa zinawakilisha nchi 13 ambazo zitakuwa wenyeji wa michuano hiyo.

Michuano ya kombe la Ulaya ya mwaka 2020, imeandaliwa kuchezwa katika miji 13 ya nchi za Ulaya, kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 60 toka kuanzishwa kwa mashindano haya, huku nusu fainali yake na fainali imeamuliwa kupigwa kwenye dimba la Wimbley jijini London.

“UEFA ilitaka mashindani ya mwaka 2020 kuwa ya aina yake kupitia mchezo tuupendao,” alisema Ceferin kwenye hotuba yake aliyoitoa kwenye ukumbi wa manispaa ya jiji la London.

“Ni namna gani tunaweza kuandaa mashiando haya ya kipekee katika kona nne tofauti za nchi za Ulaya, zaidi ya kufanya hivi?” aliuliza Ceferin.

Rais mpya wa uefa, Aleksander Ceferin, akizungumza wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya michuano ya kombe la Ulaya mwaka 2020, 21 September, 2020.
Rais mpya wa uefa, Aleksander Ceferin, akizungumza wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya michuano ya kombe la Ulaya mwaka 2020, 21 September, 2020. Reuters / Tony O'Brien Livepic

Mechi zitapigwa pia kwenye nchi za Azerbaijan, Ubelgiji, Denmark, Ujerumani, Hungary, Ireland, Italia, Uholanzi, Romania, Urusi, Scotland na Uhispania.

Ceferib aliambatana na mwenyekiti mpya wa shirikisho la mpira nchini Uingereza, Greg Clarke na meya wa jiji la London, Sadiq Khan.

Meya wa jiji la London, amepongeza uamuzi wa UEFA kufanya mashindano haya kuwa ya kipekee, na kuuchagua mji wake wa london kuwa mwenyeji wa nusu fainali na fainali ya kombe la mataifa Ulaya mwaka 2020.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza, Sam Allardayce pia alihudhuria.

Ceferin mwenye umri wa miaka 48 na wakili kutoka Slovenia, alimshinda mpinzani wake wa karibum rais wa chama cha soka cha Uholanzi, Michael van Praag kwa kura 42 kwa 13 na kushinda kwenye uchaguzi wa kupata rais mpya wa UEFA uliofanyika juma lililopita.

Ceferin ameziba nafasi iliyoachwa wazi na Michel Platin ambaye anatumikia adhabu ya kutojihusisha na soka kwa miaka minne baada ya kupatikana na hatia ya kupokea malipo ya dola milioni 2 kutoka kwa aliyekuwa rais wa Fifa, Sepp Blatter.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.