Pata taarifa kuu
SOKA-CAF

Kenya kujipima na DRC mechi ya Kimataifa ya kirafiki

Shirikisho la soka nchini Kenya FKF, limetangaza kuwa timu ya taifa Harambee Stars itachuana na Leopard ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mchuano wa Kimataifa wa kirafiki jijini Kinshasa.

Kenya ikicheza katika mchuano uliopita
Kenya ikicheza katika mchuano uliopita voiceofsport.ne
Matangazo ya kibiashara

Mchuano huu umepangwa kupigwa tarehe 4 mwezi Oktoba, baada ya makubaliano kati ya viongozi wa soka kutoka mataifa haya mawili.

DRC inatarajiwa kutumia mechi hii kujiandaa katika michuano ya hatua ya makundi kufuzu kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Kenya nayo inajiweka tayari kwa michuano ya Kimataifa ya katika siku zijazo.

Leopard, imepangwa katika kundi moja na Tunisia, Libya na Guinea katika safari ya kufuzu kombe la dunia.

Mbali na DRC, Uganda ambayo inawakilisha Afrika Mashariki katika hatua hii, imepangwa katika kundi moja na Ghana, Misri na Congo Brazaville.

Uganda Cranes ambayo imefuzu katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 38, itamenyana na Ghana katika mchuano wake wa kwanza tarehe 7 mwezi ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.