Pata taarifa kuu
US OPEN 2016

Wozniacki, Djokovic watinga hatua ya nusu fainali michuano ya US Open

Mchezaji tenesi Caroline Wozniacki, amefanikiwa kufuzu kwenye hatua ya tano ya michuano ya US Open kwa kumfunga mchezaji Anastasija Sevastova aliyecheza mchezo huo akiwa na jeraha.

Caroline Wozniacki
Caroline Wozniacki REUTERS/Shannon Stapleton
Matangazo ya kibiashara

Wozniacki alimfunga Sevastova kwa jumla ya seti mbili bila kwa matokeo ya 6-0 na 6-2, katika mchezo ambao ulikuwa wa kuvutia licha ya jeraha lililokuwa likimkabili.

Sevastova alilazimika kuufunga mguu wake kwa bandeji, baada ya kuumia wakati akijaribu kurejesha mpira aliopigiwa na Wozniacki kwenye seti ya pili.

Wozniacki sasa atacheza na Mjerumani Angelique Kerber kwenye hatua ya mzunguko wa nne wa mwisho.

Kerber alimfunga Muitaliano Roberta Vinci kwa seti mbili bila kwa matokeo ya 7-5 na 6-0.
Kwa upande wa wanaume mchezaji nambari moja kwa mchezo huo, Novak Djokovic alifanikiwa kutinga kwenye hatua ya nusu fainali ya michauno ya mwaka huu, baada ya mpinzani wake Jo-Wilfried Tosonga kujiondoa kutokana na jeraha la goti.

Novak Djokovic.
Novak Djokovic. REUTERS/Kevin Lamarque

Djokovic ambaye ni bingwa mtetezi wa michuano hii, alimfunga Tsonga kwa seti 6-3 na 6-2 kabla ya mchezaji huyo kushindwa kumudu kuendelea na mchezo.

Djokovic atakutana na Mfaransa mwingine, Gael Monfils aliyemfunga Mfaransa mwenzake Lucas Pouille kwa seti 6-4, 6-3 na 6-3.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.