Pata taarifa kuu
US OPEN 2016

Nadal, Konta watupwa nje, Djokovic atinga hatua ya 8 bora

Ndoto za mchezaji tenesi Kyle Edmund kufika hatua ya fainali ya michuano ya US Open, zimezimika baada ya kukubali kipigo kutoka kwa mchezaji nambari moja kwa mchezo huo duniani, Novak Djokovic aliyerejea baada ya kufanya vibaya kwenye michezo ya Olimpiki ya Rio, nchini Brazil.

Novak Djokovic, mchezaji nambari moja kwa ubora wa mchezo wa Tenesi duniani.
Novak Djokovic, mchezaji nambari moja kwa ubora wa mchezo wa Tenesi duniani. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Djokovic alianza vema mchezo huo toka kwenye seti ya kwanza, ambapo alifanikiwa kumfunga Edmund kwa seti tatu bila kwa matokeo ya 6-2, 6-1 na 6-4, na kufuzu hatua ya nne ya michuano ya mwaka huu.

Edmund anayeshika nafasi ya 84 kwa ubora, aliwashinda wachezaji nguli wawili kufika kwenye hatua ya 16 bora ya Grand Slams lakini alijikuta akishindwa kufua dafu mbele ya bingwa mtetezi wa taji hilo.

Kufungwa kwa Edmund kuna maanisha kuwa, Andy Murray ndiye Muingereza pekee aliyesalia kwenye michuano hiyo, huku Djokovic sasa akitarajiwa kukutana na Mfaransa, Jo-Wilfried Tsonga kwenye hatua ya 8 bora.

Rafael Nadal.
Rafael Nadal. REUTERS/Pascal Rossignol

Katika mchezo mwingine, Mfaransa Lucas Pouille alipata ushindi wa kishindi na wakihistoria, baada ya kumfunga aliyewahi kuwa bingwa mara mbili wa michuano hiyo Rafael Nadal kwenye hatua ya 16 bora.

Mchezo kati ya wachezaji hawa wawili ulilazimika kuamuliwa kwa seti ya sita, ambapo Pouille alifanikiwa kupata ushindi wa matokeo ya 6-1 2-6 6-4 3-6 7-6 (8-6) dhidi ya Nadal.

Pouille sasa atacheza na Mfaransa mwenzake Gael Monfils ambaye yeye alimfunga Marcos Baghdatis.

Kushindwa kwa Nadal, kuna maanisha kuwa mwaka 2016 ni mwaka wa kwanza toka mwaka 2004 kwa mchezaji huyu kushindwa kufika kwenye hatua ya fainali ya US Open.

Kwa upande wa wanawake, mchezaji Johanna Konta, aliondolewa kwenye michuano ya mwaka huu hatua ya 16 bora na mchezaji Anastasija Sevastova, kwa seti mbili bila kwa matokeo ya 6-4 na 7-5.

Johanna Konta.
Johanna Konta. Reuterss/Issei Kato

Konta alipambana kurejea kwenye seti ya pili hadi kufikia alama 5-5 kutoka alama 4-1 lakini alijikuta akishindwa kumudu kasi ya Sevastova na kushindwa kwenye seti hiyo.

Sevastova ambaye alitangaza kustaafu mchezo huo mwaka 2013 kabla ya kutangaza kurejea, atacheza na Caroline Wozniacki kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya mwaka huu.

Konta alikuwa akijaribu kupambana na kuwa Muingereza wa kwanza kufika kwenye hatua ya robo fainali ya taji kubwa la “Grand Slams” jijini New York toka alipofanya hivyo Muingereza, Jo Durie mwaka 1983.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.