Pata taarifa kuu
UEFA

Ratiba ya mechi za makundi klabu bingwa Ulaya yawekwa wazi

Shirikisho la kabumbu barani Ulaya, UEFA, limetoa ratiba ya mechi za makundi ya michuano ya klabu bingwa Ulaya, huku mabingwa Real Madrid wakikumbana uso kwa uso kwenye mchezo wao wa kwanza na klabu ya Borrusia Dortmund.

Picha ikionesha maofisa wa Uefa wakati wakichezesha droo ya makundi
Picha ikionesha maofisa wa Uefa wakati wakichezesha droo ya makundi REUTERS/Eric Gaillard
Matangazo ya kibiashara

Klabu ya Ufaransa ya Paris Saint-Germain imepangwa katika kundi A ikiwa pamoja na Arsenal ya Uingereza, FC Basel ya Uswis na Ludogorets Razgrad ya Bulgaria.

Kundi B lina timu za Benfica ya Ureno, Napoli ya Italia, Dynamo Kyiv ya Ukraine na Beşiktaş ya Uturuki.

Kundi C lina timu za Barcelona ya Uhispania, Manchester City ya Uingereza, Borussia Mönchengladbach ya Ujerumani na Celtic ya Scotland.

Kundi D lina timu za Bayern München ya Ujerumani, Atlético Madrid ya Uhispania, PSV Eindhoven ya Uholanzi na Rostov ya Urusi.

Kundi E lina timu za CSKA Moskva ya Urusi, Bayer Leverkusen ya Ujerumani, Tottenham Hotspur ya Uingereza na Monaco ya Ufaransa.

Kundi F limejumuisha timu za Real Madrid ya Uhispania ambao ndio mabingwa,  Borussia Dortmund ya Ujerumani, Sporting CP ya Ureno na Legia Warszawa ya Poland.

Kundi G lina timu za Leicester City ya Uingereza, Porto ya Ureno, Club Brugge ya Ubelgiji na FC København ya Denmark.

Kundi H lina timu za Juventus ya Italia, Sevilla ya Uhispania, Lyon ya Ufaransa na Dinamo Zagreb ya Croatia.

Mechi za kwanza za makundi zinatarajiwa kupigwa kuanzia September 13 na 14.

Katika hatua nyingine, tuzo ya mchezaji bora wa kike na wakiume zilitolewa kwenye sherehe za upangaji wa makundi hayo, ambapo kwa upande wa wanaume, mshambuliaji wa Real Madrid, Christian Ronaldo alishinda tuzo hiyo, huku kwa upande wa wanawake mchezaji wa Lyon ya Ufaransa, Ada Hegerberg.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.