Pata taarifa kuu
SOKA-AFCON

Michuano ya marudiano kufuzu AFCON kwa wachezaji wasiozidi miaka 17 kupigwa

Michuano ya marudiano ya mchezo wa soka hatua ya mzunguko wa pili kufuzu katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 17 mwaka ujao nchini Madagascar zinachezwa mwishoni mwa juma hili.

Nembo ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF
Nembo ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF cafonline
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumamosi, Msumbiji watakuwa wenyeji wa Comoros jijini Maputo baada ya Msumbuji kufungwa kwa mabao 2-1.

Vijana wa Niger nao watakuwa wenyeji wa Nigeria baada ya kupoteza mchuano wa kwanza bao 1-0, huku Ivory Coast na Benin wakimenyana baada ya sare ya bao 1 kwa 1 wiki mbili zilizopita.

Ratiba ya Jumamosi Agosti 19 2016

  • Kenya vs Cameroon
  • Msumbiji vs Comoros
  • Gabon vs Algeria
  • Angola vs Mauritius
  • Niger vs Nigeria
  • Burkina Faso vs Ghana
  • Cote d'Ivoire vs Benin
  • Senegal vs Tunisia

Vijana wa Kenya watashuka uwanjani baada ya kipigo kizito cha mabao 7-0 katika mechi ya kwanza ugenini.

Matumaini ya Kenya kufuzu katika mzunguko wa mwisho hayapo kutokana na wingi wa mabao waliyofungwa na itakuwa ni vigumu kufunga angalau mabao 9-0.

Siku ya Jumapili, Tanzania ambayo ililazimisha sare ya bao 1 kwa 1 na Afrika Kusini, itarudiana na wapinzani wao katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Ratiba ya mechi zingine za Jumapili;

  • Chad vs Mali
  • Misri vs Ethiopia
  • Guinea vs Morocco
  • Namibia vs Congo
  • Sudan vs Zambia

Mataifa 14 yatafuzu katika mzunguko wa tatu.

Mataifa nane yatafuzu katika fainali hiyo itakayofanyika mwezi Juni mwaka ujao.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.