Pata taarifa kuu
RIO OLIMPIKI 2016

Brazil yatinga robo fainali, Argentina yatupwa nje

Timu ya taifa ya Brazili ya mpira wa miguu, vijana chini ya umri wa miaka 23, imefanikiwa kutinga kwenye hatua ya robo fainali ya michezo ya Olimpiki ya Rio, baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Denmark. 

Wachezaji wa Brazil, wakiwa wanashangilia baada ya timu yao kupata nafasi ya kicheza hatua ya robo fainali ya michezo ya Rio, Brazil, 11 Agosti, 2016.
Wachezaji wa Brazil, wakiwa wanashangilia baada ya timu yao kupata nafasi ya kicheza hatua ya robo fainali ya michezo ya Rio, Brazil, 11 Agosti, 2016. REUTERS/Fernando Donasci
Matangazo ya kibiashara

Mchezaji Gabriel Barbosa aliipatia timu yake bao la kuongoza kabla ya mchezaji mpya wa Manchester City, Gabriel Jesus kuifungia timu yake bao la pili kwa mkwaju wa nje ya eneo la 18.

Mchezaji Luan aliiandikia timu yake bao la tatu kabla ya mpira uliopigwa na Barbosa kumgonga mchezaji wa Denmark na kuandika bao la nne na la ushindi, lililotosha kuifanya Brazil kuongoza kwenye kundi lake la A.

Hata hivyo timu ya vijana ya Argentina pamoja na mabingwa wa michezo ya Olimpiki ya London mwaka 2012, walishindwa kufurukuta na kujikuta wakiaga michuano ya mwaka huu.

Argentina ilimaliza kwenye nafasi ya tatu kwenye kundi D baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Honduras, huku Mexico wakifungwa na Korea Kusini kwa bao 1-0.

Kwa matokeo haya, Brazil itacheza na Colombia kwenye mchezo wa robo fainali, huku Denmark yenyewe iliyosonga mbele licha ya kufungwa, wamemaliza kwenye nafasi ya pili.

Ujerumani yenyewe ilimaliza kwa kishindoi kwenye kundi lake, baada ya kuisambaratisha Fiji kwa jumla ya mabao 10-0.

Ureno ilimaliza ya kwanza kwenye kundi D baada ya kutoka sare na Algeria ya bao 1-1, kwenye dimba la Belo Horizonte.

Colombia yenyewe ilisonga mbele baada ya kuwafunga vinara wa kundi B timu ya taifa ya Nigeria kwa mabao 2-0, matokeo yaliyomaliza na kuzima ndoto ya Japan kusonga mbele kwa kumaliza kwenye nafasi ya tatu licha ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sweden.

Mechi za robo fainali zitakuwa kama ifuatavyo, Brazil v Colombia; Portugal v Germany; South Korea v Honduras; Nigeria v Denmark.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.