Pata taarifa kuu
FIFA-NIGERIA

Rais wa FIFA Gianni Infantino ziarani nchini Nigeria

Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Gianni Infantino na Katibu Mkuu Bi. Fatma Samoura wanazuru nchini ya Nigeria kwa ziara ya siku tatu.

Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino (Katikatai) akiwa na viongozi wa soka nchini Nigeria
Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino (Katikatai) akiwa na viongozi wa soka nchini Nigeria FIFA
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao waliwasili jijini Abuja mwishoni mwa juma lililopita na kukaribishwa na rais wa Shirikisho la soka nchini humo NFF Amaju Pinnick.

Hii ni ziara yake ya pili barani Afrika, tangu kuchaguliwa kwake kuwa rais wa FIFA, baada ya kufanya ziara nyingine kama hii nchini Sudan Kusini mwezi Machi kufungua Ofisi ya Shirikisho la soka nchini humo jijini Juba.

Infantino pia amekutana na viongozi wa vyama vya soka kutoka mataifa ya Afrika  kujadili maswala mbalimbali ya maendeleo ya soka katika nchi zao.

Viongozi wa soka kutoka mataifa hayo ya bara Afrika ni pamoja na:- Kwesi Nyantakyi (Ghana), Lamin Kaba Bajo (The Gambia), Isha Johansen (Sierra Leone), Musa Bility (Liberia), Juneidi Basha Tilmo (Ethiopia), Nick Mwendwa (Kenya), Andrew Chamanga(Zambia),

Wengine ni pamoja na:- Philip Chiyangwa (Zimbabwe), Frans Mbidi (Namibia), Chabur Goc Alei (South Sudan), Walter Nyamilandu (Malawi), Abdiqani Said Arab (Somalia), Vincent Nzamwita (Rwanda), Moses Magogo (Uganda), Jamal Malinzi (Tanzania), Augustin Senghor (Senegal) and Souleman Waberi (Djibouti).

Rais huyo wa FIFa na viongozi hawa wa soka wanakutana pia na rais Muhamadu Buhari katika Ikulu ya Abuja.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.