Pata taarifa kuu
Rio 2016-URUSI

RIO-2016: Urusi yatakiwa kuondolewa katika Michezo ya Olimpiki

Mashrika 14 yanayopambana dhidi ya madawa ya kusisimua mwili, ikiwa ni pamoja na USADA kutoka Maekani na NADA la Ujerumani, alhamisi hii, walimtumia barua ya pamoja Mkurugenzi Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki (IOC), Thomas Bach yakimtaka kuifuta Urusi katika mashindano Michezo ya Olimpiki 2016.

Mashirika 14 yanayopambana dhidi ya madawa ya kusisimua mwili yaitaka Urusi kuchukuliwa vikwazo.
Mashirika 14 yanayopambana dhidi ya madawa ya kusisimua mwili yaitaka Urusi kuchukuliwa vikwazo. (Photo : Reuters)
Matangazo ya kibiashara

Katika mwanga wa hitimisho la ripoti inayojulikana kwa jina la McLaren iliyokubaliwa na shirika la kimataifa linalopambana dhidi ya madawa ya kusisimua mwili (WADA) na Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya OlimpikiI (IOC), na ambapo muda wa kutosha ulitolewa kabla ya Michezo ya Olimpiki ya mjini Rio de Janeiro, tunaamini ni sahihi na nimuhimu kwa kamati ya Michezo ya Olimpiki kuchukua hatua thabiti ili kulinda Mkataba wa Olimpiki na uadilifu wa mashindano ya Michezo ya Olimpiki ya mjini Rio de Janeiro, " imebaini barua hiyo, inayopatikana kwenye tovuti ya Kituo cha Canada kwa ajili ya maadili katika Michezo, moja ya mashirika yaliyotia saini.

"Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki hawezi, haipaswi kuagiza majukumu hayo kwa wengine. Hivyo basi, tunaomba Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki kutumia mamlaka yake kwa niaba ya Mkataba wa Olimpiki (...) kwa kuisimamisha Kamati ya Olimpiki ya Urusi na kuifuta Urusi katika mashindano ya Michezo ya Olimpiki ya mjini Rio de Janeiro 2016, " barua hiyo imeongeza.

Wakurugenzi wa mashirika hayo 14 yaliyosaini barua hiyo (Ujerumani, Austria, Canada, Denmark, Misri, Uhispania, Marekani, Finland, Japan, Uholanzi, New Zealand, Norway, Sweden na Switzerland) Pia walitoa wito wa kuundwa kwa "kikosi kazi" itakachowajibika kwa ajili ya kuweka vigezo na ambavyo wanariadha wa Urusi wanaweza kuokolewa mmoja mmoja kwa kushiriki katika mashindano ya Michezo ya Olimpiki ya mjini Rio de Janeiro chini ya bendera isiyoegemea nchi yoyote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.