Pata taarifa kuu
EURO 2016

Ufaransa kusaka ushindi dhidi ya timu" ngumu" ya Iceland

Robo fainali ya mwisho kuwania taji la bara Ulaya katika mchezo wa soka inachezwa leo usiku kuanzia saa nne usiku, saa za Afrika Mashariki.

Matangazo ya kibiashara

Wenyeji wa michuano hii Ufaransa watachuana na Iceland katika uwanja wa Stade de France jijini Paris, mchuano ambao unatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki.

Ufaransa ilifuzu katika hatua hii baada ya kumaliza ya kwanza katika kundi A kwa alama 7 mbele ya Uswizi, Albania na Romania.

Iceland nayo ilimaliza ya pili katika kundi lake la F kwa alama 5 nyuma ya Hungary ambayo iliondolewa katika hatua ya 16 bora.

Mchezaji wa Ufaransa Samuel Umtiti anatarajiwa kuichezea timu yake kwa mara ya kwanza kuchukua nafasi ya Adil Rami ambaye amefungiwa kucheza katika mchuano huu wa leo, huku N'Golo Kante akifungiwa mchezo mmoja.

Timu ya taifa ya Ufaransa
Timu ya taifa ya Ufaransa weltsport.net

Historia ya timu hizi mbili inaonesha kuwa, Ufaransa haijafungwa na Iceland katika michuano 11 ambazo timu hizi mbili zimekutana.

Iceland wamepoteza mechi zake zote 6 walizocheza ugenini dhidi ya Ufaransa jijini Paris, lakini imefunga mabao matano na kufungwa mabao 22.

Timu ya taifa ya Iceland
Timu ya taifa ya Iceland Reuters

Mara ya mwisho kwa mataifa haya kukutana, Ufaransa ilishinda kwa mabao 3 kwa 2.

Wachambuzi wa soka wanasema mchuano huu utakuwa mgumu na Iceland inatarajiwa kuleta ushindani mkali.

Siku ya Jumamosi, Ujerumani ilifuzu katika hatua ya nusu fainali baada ya kuishinda Italia mabao 6 kwa 5 baada ya kutoka sare ya bao 1 kwa 1 katika muda wa kawaida na ule wa ziada na sasa inasubiri mshindi wa leo kutafuta nafasi ya kucheza fainali siku ya Alhamis juma lijalo.

Nusu fainali ya pili ni kati ya Ureno na Wales siku ya Jumatano huku fainali ikipangwa kufanyika Jumapili ijayo katika uwanja wa Stade de France.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.