Pata taarifa kuu
RIADHA

IOC yasema haina imani na wanariadha wa Urusi na Kenya

Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki IOC inasema mifumo mibaya ya kukabiliana na wanamichezo wanaotumia dawa zilizopigwa marufuku za kuongeza nguvu mwilini nchini Urusi na Kenya, zimesababisha hata wanariadha wasiotumia dawa hizo kutiliwa shaka.

Rais wa  IOC Thomas Bach (K) akiwa na naibu wake  John Coates (KL) na rais wa Kamati ya Olimpiki ya Japan  Tsunekazu Takeda
Rais wa IOC Thomas Bach (K) akiwa na naibu wake John Coates (KL) na rais wa Kamati ya Olimpiki ya Japan Tsunekazu Takeda Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Kamati hiyo Thomas Bach amesema kwa sababu Shirika la Kimataifa linalopambana na matumizi ya dawa hizo  WADA, tayari liliwahi kutangaza kuwa mataifa hayo mawili hayashirikiani nayo, na sasa inakuwa vigumu kuwaamini wanariadha wote wa nchi hizo ikiwa hawana hatia.

Hata hivyo, imekubaliwa kuwa  mwanariadha mmoja mmoja wa Urusi na Kenya ambaye atakuwa amebainika hajatumia dawa hizo ataruhusiwa kushiriki michezo ya Olimpiki nchini Brazil mwezi Agosti chini ya bendera michezo hiyo.

Hii inamaanisha kuwa wanariadha hao kutoka nchi hizo watapimwa kabla ya kushiriki katika michezo hiyo hasa wale kutoka Kenya siku kadhaa tu baada ya serikali kuwasilisha sheria ya kukabiliana na matumizi ya dawa hizi.

Mbali na hilo, Kamati hiyo ya IOC wameunga mkono uamuzi wa Shirikisho la riadha dunia IAAF kusisitiza kuwa Urusi haitashiriki katika michezo hiyo, uamuzi wao Urusi umekosoa vikali.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.