Pata taarifa kuu
KOMBE LA SHIRIKISHO

Mechi za kombe la shirikisho barani Afrika kupigwa mwishoni mwa juma

Mechi za kombe la shirikisho barani Afrika zinatarajiwa kuendelea tena mwishoni mwa juma hili ambapo zimefikia kwenye hatua ya makundi.

Kombe la shirikisho barani Afrika
Kombe la shirikisho barani Afrika Bin Katanga
Matangazo ya kibiashara

Lakini wakati mechi hizi zikitarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa juma, baadhi ya vilabu vinavyoshiriki viko kwenye hati hati ya kucheza baadhi ya mechi zake kutokana na ukata unaovikabili.

Mwingoni mwa timu ambazo zinakabiliwa na ukata, ni klabu ya Medeama ya nchini Ghana, ambayo yenyewe imesafir kuelekea nchini DRC kucheza na waliowahi kuwa mabingwa wa kombe la klabu bingwa Afrika, TP Mazembe.

Medeama imesafiri kuelekea nchini DRC ikiwa na matumaini ya kufanya vyema kwenye mchezo huo, licha ya hali ngumu ya ukata unaoikabili timu hiyo, ambapo kwa nyakati fulani imekuwa ngumu kwa timu hiyo kupata mahitaji muhimu.

Rais wa Medeama, Moses Armah amesema kuwa wao wanaenda nchini DRC kwa lengo moja tu la kupambana na kuhakikisha wanaifunga TP Mazembe, lakini akasema tatizo kubwa linaloikabili timu yake kwa sasa ni namna watakavyosafiri kutokana na kukosa fedha.

Medeama ambayo haijwahi kutwaa taji lolote la michuano ya Afrika, italazimika kusafiri kwenda nchini DRC, Algeria na Tanzania kwenye hatua ya makundi, na ikiwa itamaliza kwenye nafasi ya mwisho kwenye kundi lake, itajinyakulia zawadi ya kitita cha dola za Marekani elfu 15.

Armah amesema kuwa tayari alishawasiliana na wizara ya michezo nchini Ghana pamoja na shirikisho la mpira barani Afrika CAF kuangalia uwezekano wa kusaidia na kuongeza kuwa maombi yao kwa sehemu kubwa yamefanikiwa na wanachowaza sasa ni kuanza safari ya kuelekea DRC.

Baadhi ya wachezaji kwenye timu hiyo ambao awali waliahidiwa kitita cha dola za Marekani 2000 ikiwa wangeifunga klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, hawajalipwa na kwa sasa uwezekano ni mdogo wa kupata fedha hizo.

Mechi nyingine ambazo zitapigwa mwishoni mwa juma, ni pamoja na klabu ya Novices Mouloudia Bejaia ya Algeria ambayo yenyewe itakuwa nyumbani kuwakabili mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania Young Africans katika mchezo wa kundi A.

Kwenye mechik ya kundi B, mabingwa wa kombe la shirikisho mwaka 2010, FUS Rabat itawakaribisha Kawkab Marrakech ya Morocco, huku mabingwa watetezi wa kombe hilo, Etoile Sahel ya Tunisia itakuwa inawakaribisha Al Ahli Tripoli ya Libya.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.