Pata taarifa kuu
COPA AMERIKA 2016

Marekani yatinga nusu fainali, kuzisubiri Argentina au Venezuela

Michuano ya kombe la Copa Amerika imeendelea kushika kasi, ambapo wenyeji wa michuano ya mwaka huu, timu ya taifa ya Marekani, imekuwa timu ya kwanza kutinga kwenye hatua ya nusu fainali.

Mchezaji wa Marekani, Clint Dempsey, akiruka juu kufunga goli kwa timu yake
Mchezaji wa Marekani, Clint Dempsey, akiruka juu kufunga goli kwa timu yake Joe Nicholson-USA TODAY Sports
Matangazo ya kibiashara

Kwenye mchezi huo, Marekani ilibidi ifanye kazi ya ziada na kufanikiwa kupata goli la ushindi kwenye dakika za lala salama, na kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ecuador.

Ushindi huu dhidi ya Ecuador, unaifanya Marekani kufuzu kwenye hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza toka mwaka 1995.

Wachezaji Clint Dempsey na Gyasi Zardes ndio walikuwa mashujaa wa Marekani, huku bao pekee la Ecuador likifungwa na mchezaji Michael Arroyo, huku mechi yenyewe ikishuhudia kila timu ikipoteza mchezaji wake kwa kutolewa kwa kadi nyekundu.

Ecuador ilirejea kwenye mchezo kwa nguvu baada ya wachezaji Antonio Valencia na Jermaine Jones kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika dakika ya 51 ya mchezo, lakini hata hivyo Marekani sasa itacheza mchezo wake wa nusu fainali na kati ya timu ya Argentina au Venezuela, mjini Houston, Jumanne ya wiki ijayo.

Kocha mkuu wa Marekani, Jurgen Klinsmann, amesema kuwa wametoka mbali toka hatua ya makundi na kwamba wanazidi kupata nguvu kadiri wanavyosonga mbele kwenye hatua inayofuata.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.