Pata taarifa kuu
MUHAMMAD ALI

Dunia kumuaga Muhammad Ali

Maelfu ya raia kutoka mataifa mbalimbali duniani, wameshirika kwenye maombi ya pamoja ya kiislamu, kumkumbuka Muhammad Ali nguli wa masumbwi aliyefariki juma moja lililopita. 

Mfano wa gloves alizokuwa akitumia Muhammad Ali zikiwa kwenye makazi yake ya zamani, Louisville, Kentucky.
Mfano wa gloves alizokuwa akitumia Muhammad Ali zikiwa kwenye makazi yake ya zamani, Louisville, Kentucky. Reuters/Lucas Jackson
Matangazo ya kibiashara

Maombi haya yaliyofanyika kwenye msikiti wa Louisville, alikozaliwa Muhammad Ali na kuishi huko kwa muda mrefu, yalikuwa ni sehemu ya ibada ya siku mbili ya kumkumbuka na kutoa heshima za mwisho kwa mwanamasumbwi huyu aliyekuwa kipenzi cha dunia na shujaa aliyetetea haki za binadamu.

Wanaume, wanawake na mamia ya familia walifurika kwenye ukumbi wa Freedom, mjini Kentucky kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu Muhammad Ali kabla ya maziko yanayotarajiwa kufanyika hii leo.

Sherehe fupi iliyofanyika kwenye mji wa Louisville, ilikuwa ni sehemu ya kuzindua siku mbili za ibada za pamoja kwa dini ya kiislamu na Kikristo kama alivyotaka kufanyika marehemu muhammad Ali kabla ya kufariki kwake.

Baadhi ya waombolezaji wakitembelea nyumba ya makumbusho aliyoishi Muhammad Ali, Louisville, Kentucky
Baadhi ya waombolezaji wakitembelea nyumba ya makumbusho aliyoishi Muhammad Ali, Louisville, Kentucky 路透社

Imamu aliyeoongoza ibada ya kumuombea Muhammad Ali, amesema kuwa alifurahishwa kuona watu wa mataifa mbalimbali wakikusanyika bila kujali tamaduni, rangi, dini wala itikadi na kwamba ulikuwa ni wakati muafaka kukumbuka mazuri aliyoyafanya mwanamasumbwi huyu.

Hii leo ibada ya mazishi itafanyika, ambapo viongozi kadhaa wa dunia wanatarajiwa kuhudhuria mazishi ya Ali aliyefariki akiwa na umri wa miaka 74, ambapo anatajwa na kila raia kuwa alikuwa mtu wa aina yake yake.

Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton atahudhuria ibada ya mazishi ya Muhammad Ali ambapo pia atasoma wasifu wa marehemu, akisindikizwa na wakuu mbalimbali wa dunia akiwemo rais wa Uturuki, Racep Tayyip Erdogan na mwanamfalme wa Jordan miongoni mwa wanaotarajiwa kuhudhuria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.