Timu 4 zatinga nusu fainali
Hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imepigwa Alhamisi hii, Aprili 14 kwa michezo minne.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Sevilla imeiondoa Athletic Bilbao kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya mechi ya awali na ya maurudiano timu zote mbili kujikuta zimetoka sare ya kufungana jumla ya mabao 3-3 baada ya kila timu kushinda 2-1 mechi ya nyumbani.
Villarreal imeinyeshea mvua ya mabao Sparta Praga kwa kuichapa 4-2, huku Liverpool ikiilamba Borrussia Dortmund mabao 4-3.
Magoli ya Liverpool yamewekwa wavuni na Divock Origi, Philippe Coutinho, Mamadou Sakho na Dejan Lovren.
Kwa upande wa Dortmund, wachezaji Henrikh Mkhitaryan, Pierre-Emerick Aubameyang na Marco Reus waliliona lango la Liverpool.
Sevilla, Villarreal, Liverpool na Shakhtar Donetsk wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Ulaya.