Pata taarifa kuu
KENYA-SOKA

Harambee Starlets kushiriki michuano Cameroon

Kenya itashiriki katika michuano ya soka ya Afrika kwa upande wa wanawake kwa mara ya kwanza, nchini Cameroon kati mwezi Novemba na Disemba mwaka huu.

Nchini Congo-Brazzaville, Nzango, ni mchezo wa wanawake na wasichana unaochezwa wakiimba.
Nchini Congo-Brazzaville, Nzango, ni mchezo wa wanawake na wasichana unaochezwa wakiimba. Source : https://www.youtube.com/
Matangazo ya kibiashara

Warembo wa Harambee Starlets waliweka historia siku ya Jumanne kwa kufuzu katika michuano hiyo ya Afrika kwa sababu ya bao la ugenini baada ya kutoka sare ya bao 1 kwa 1 na Algeria jijini Nairobi.

Mchuano wa mzunguko wa kwanza jijini Algers, Kenya ililazimisha sare ya mabao 2 kwa 2.

Kenya sasa inajiunga na wenyeji Cameroon ambao mwaka 2014 walimaliza wa pili lakini pia mwaka 1991 na 2004.

Misri nayo imefuzu kwa mara ya pili baada ya kushiriiki mara ya kwanza mwaka 1998 na kuondolewa katika hatua ya makundi.

Mabingwa wa mwaka 2008 na 2015, Equitorial Guinea nao wamejikatia tiketi ya kucheza katika fainali hii ambayo wamecheza mara tano sasa.

Nigeria ambao ni mabingwa watetezi na ambao wameshinda taji hili mwaka 1991, 1995, 1998, 2000, 2004, 2006, 2010 na 2014 wanashiriki kwa mara ya 12.

Huku Afrika Kusini nayo imefuzu kwa maraya 11 na Zimbabwe iliyomaliza nafasi ya nne mwaka 2000 itacheza kwa mara ya nne.

Mataifa haya manane yatajumuishwa katika makundi mawili, kila kundi likiwa na timu nne.

Timu mbili za kwanza katika kila kundi zitafuzu katika hatua ya nusu fainali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.