Pata taarifa kuu
FIFA-SOKA-UFISADI

Hatma ya Blatter na Platini mbele ya Kamati ya Nidhamu

Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka duniani FIFA inapendekeza kuwa rais wa Shirikisho hilo Sepp Blatter aondoke madarakani kwa siku tisini.

Joseph Blatter na Michel Platini Mei 25, 2015 jijini Zurich.
Joseph Blatter na Michel Platini Mei 25, 2015 jijini Zurich. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Lakini taarifa hii imekanushwa harakaJumatano jioni na Richard Cullen, mwanasheria wa Sepp Blatter, mwenye umri wa miaka 79: " Rais Blatter hajapata taarifa ya mapendekezo yaliyotolewa dhidi yake ", amesema Richard Cullen katika taarifa aliyotoa.

Hatua hii inakuja baada ya viongozi wa Mashtaka nchini Uswizi kuanza kumchunguza Blatter kwa tuhma za kutoa malipo yasiyokuwa rasmi kwa rais wa Shirikisho la soka barani Ulaya Uefa lakini kutoa saini mkataba ambao haukuwa manufaa kwa FIFA.

Blatter ameendelea kukanusha tuhma hizo na kusema hana hatia yoyote na hawezi kujizulu kabla ya tarehe 26 mwezi Februari mwaka ujao siku ambayo uchaguzi mpya wa FIFA utakapofanyika.

Michel Platini naye amesema fedha alizolipwa alikuwa amezifanyia kazi na hajahusika na ufisadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.