Pata taarifa kuu
CHAN-SOKA

CHAN: timu tatu zafuzu katika mzunguko wa pili

Timu ya taifa za soka za Uganda, Ethiopia na Burundi zimefuzu katika mzunguko wa pili kutafuta nafasi ya kucheza katika fainali za matifa bingwa barani Afrika baina ya wachezaji wanaocheza soka nyumbani katika michuano ya CHAN itakayofanyika mwaka ujao nchini Rwanda.

Timu ya taifa ya soka ya Burundi (Intamba).
Timu ya taifa ya soka ya Burundi (Intamba). youtube
Matangazo ya kibiashara

Uganda ilifuzu kwa jumla ya mabao 4 kwa 1 baada ya kuiondoa Tanzania ambayo iliilazimisha sare ya bao 1 kwa 1 katika mchuano wa marudiano mwishoni mwa juma jijini Kampala.

Ethiopia nayo ilifuzu baada ya ushindi wa mabao 2 kwa 0 dhidi ya Harambee Stars ya Kenya na mwisho mwa juma lililopita katika mchuano wa marudiano jijini Nairobi, mchuano huo ulimalizika kwa sare ya kutofungana.

Burundi nayo ilifanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya ushindi wa mabao 4 kwa 1 dhidi ya Djibouti baada ya kupata ushindi wa mabao 2 kwa 0 Jumamosi iliyopita.

Kwa matokeo hayo, Uganda itamenyana na Sudan, huku Burudi ikicheza na Ethiopia.
Mechi hizi zitachezwa nyumbani na ugenini na washindi watafuzu katika michuano ya CHAN kuwakilisha eneo la Afrika Mashariki mwakani.

Rwanda imefuzu kwa sababu wao ni wenyeji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.