Pata taarifa kuu
TANZANIA-SOKA

Mashabiki wa Taifa Stars wakata tamaa

Timu ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, imeanza vibaya michuano ya kuwania ubingwa wa soka baina ya mataifa ya Kusini mwa Afrika inayoendelea nchini Afrika Kusini baada ya kufungwa na Swaziland bao 1 kwa 0.

Mashabiki wa Taifa Stars wakati ilipokua ikifuana na Cote d'Ivoire  June 16 mwaka 2013.
Mashabiki wa Taifa Stars wakati ilipokua ikifuana na Cote d'Ivoire June 16 mwaka 2013. YouTube
Matangazo ya kibiashara

Swaziland ambao wanaorodheswa chini ya Tanzania katika orodha ya mataifa bora ya Shirikisho la soka duniani FIFA waliwashangaza mashabiki kwa kupata ushindi huo muhimu kupitia bao la mchezaji Sifiso Mabila.

Timu hizi mbili zilikutana mara ya mwisho mwaka uliopita katika mchuano wa Kimataifa wa kirafiki na kutoka sare ya kufungana bao 1 kwa 1.

Taifa Stars ambayo imealikwa katika michuano hiyo sasa ina kazi kubwa kesho Jumatano katika mchuano wake dhidi ya Madagascar ili kuwa na matumaini ya kusonga mbele.

Baadhi ya mashabiki wa Taifa Stars jijini Dar es salaam wanasema hawaoni timu yao ikifika mbali kwa kile wanachokisema kuwa kocha Mart Nooij hakukiteua kikosi sahihi kushiriki katika michuano hii.

“ Kwa kweli niliuona mchuano huo, sisi tulifanikiwa tu kulenga golini mara tatu kinyume na Swaziland ambao walikuwa wametulia”, amesema Emmanuel Richard mkaazi wa Dar es salaam.

“ Sioni tukifika mbali tukiendelea kucheza kama ilivyokuwa jana”, ameongeza.

Madagascar wanaongoza kundi la B kwa alama 3 wakifuatwa na Swaziland huku Lesotho na Tanzania zikikosa alama.

Siku ya Jumanne usiku michuano ya kundi la A, zitarejelewa na Ushelisheli wanamenyana na Zimbabwe kuanzia saa kumi na mbili kamili jioni saa za Afrika Mashariki lakini baadaye saa mbili na nusu usiku Namibia watamenyana na Mauritius.

Mshindi katika kila kundi atafuzu katika hatua ya robo fainali.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.