Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-NIGERIA-SOKA

Serero na Mahlangu watakiwa kujiunga na Bafana Bafana

Kocha wa Timu ya taifa ya soka ya Afrika Kusini Bafana Bafana, Ephraim Shakes Mashaba, amewaita viungo wa kati Thulani Serero na May Mahlangu kucheza katika michuano miwili ya kirafiki dhidi ya Swaziland na Nigeria.

Timu ya taifa ya soka ya Afrika Kusini bafana bafana.
Timu ya taifa ya soka ya Afrika Kusini bafana bafana. AFP/Alexander Joe
Matangazo ya kibiashara

Wachezaji hao wawili wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya waliachwa na kocha Mashaba wakati wa michuano ya mataifa bingwa barani Afrika nchini Equitorial Guinea mwezi Januari kwa baada ya kususia mazoezi ya timu ya taifa.

Mechi hizo zitachezwa tarehe 25 dhidi ya Swaziland na tarehe 29 dhidi ya Nigeria kwa maandalizi ya michuano ya kufuzu kushiriki katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 na mwenyeji wa michuano hii atafahamika tarehe 8 mwezi ujao.

Wakati huo huo timu ya taifa ya soka ya Bolivia, imekataa kusafiri kuja nchini Nigeria kucheza na Super Eagles katika mchuano wa Kimataifa wa kirafiki kwa kuhofia usalama wao.

Mchuano huo ulikuwa umepangwa kuchezwa katika mji wa Uyo Kusini mwa nchi hiyo Alhamisi ijayo.

Vongozi wa Shirikisho la soka nchini humo NFF wanasema watatafuta nchi nyingine kuchukua nafasi ya Bolivia.

Haya yakijiri kuna mchuano wa nusu fainali, kuwania taji la soka baina ya vijana wasiozidi miaka 20 inyaoendelea nchini Senegal.

Nigeria itachuana na Ghana mechi itakayochezwa kuanzia saa mbili usiku saa za Afrika Mashariki.

Kesho itakuwa ni zamu ya Mali na wenyeji Senegal. Fainali itachezwa siku ya Jumapili.

Mbali na kutafuta ubingwa wa Afrika, mataifa yote haya yaliyofika katika hatua ya nusu fainali yamefuzu katika michuano ya kombe la dunia baina ya vijana itakayochezwa nchini New Zealand mwezi Juni mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.