Pata taarifa kuu
AFRIKA-CAF-SOKA-AFCON 2015-MICHEZO

AFCON 2015: michuano ya mwisho yachezwa Jumatano hii

Leo Jumatano jioni Novemba 19 kutakuwa na michuano ya mwisho ya mchezo wa soka kufuzu katika fainali za mwaka ujao kutafuta bingwa wa Afrika nchini Equitorial Guinea.

Wakati wa mchuano wakufuzu katika kutafuta bingwa wa Afrika nchini Equitorial Guinea kati ya  Côte d'Ivoire na Sierra Leone.
Wakati wa mchuano wakufuzu katika kutafuta bingwa wa Afrika nchini Equitorial Guinea kati ya Côte d'Ivoire na Sierra Leone. REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Afrika Mashariki macho yote yatakuwa kwa Uganda Cranes ambao wapo mjini Cassablanca nchini Morroco kumenyana na Guinea, na wanahitaji ushindi au sare ili kufuzu katika michuano hiyo.

Timu ya Uganda na Guinea zote zina alama saba katika kundi lao.

Mara ya mwisho kwa Uganda Cranes kucheza katika michuano hii mikubwa barani Afrika ilikuwa ni ziadi ya miaka 30 iliyopita.

Nayo timu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itakuwa nyumbani katika uwanja wa Kimataifa wa Tata Raphael jijini Kinshasa kucheza na Sierra Leone.

Leopard ambayo ina alama sita katika kundi lake, inahitaji kupata ushindi wa mabao mengi leo jioni na kuomba kuwa Cameroon inawafunga Cote d'Ivoire, ili kufuzu kwenda Equitorial Guinea.

Mechi nyingine muhimu ni pamoja na mabingwa watetezi Nigeria ambao wanahitaji kuishinda Afrika Kusini, ili kufuzu sawa na Congo Brazaville inayocheza na Sudan jijini Khartoum.

Malawi na Mali pia watakuwa wanatafuta nafasi ya kufuzu, Malawi inahitaji ushindi dhidi ya Ethiopia jijini Addis Ababa, huku Mali wakiwa nyumbani jijini Bamako kuvaana na Algeria.

Miongoni mwa Mataifa yaliyofuzu hadi sasa ni pamoja na Algeria, Afrika Kusini, Burkina Faso, Cape Verde na Zambia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.