Pata taarifa kuu
PSG-Ligi ya Ufaransa

PSG yasubiri kuwapokea wachezaji wake wa kimataifa

Mshambuliaji wa klabu ya Paris Saint Germain kutoka Uruguay, Edinson Cavani, ambaye hakushiriki mazoezi jumatatu hii, atajiunga katika na Klabu yake ijumaa, siku ambayo Paris Saint Germain itajielekezaHon Kong, kushiriki michuano ya kikanda, PSG imethibitisha.

Wachezaji wa Paris Saint-Germainwakifurahia kutwaa kombe la klabu bingwa nchini Ufaransa (Coupe de France) baada ya kuifunga Monaco bao 1-0 mwaka 2010..
Wachezaji wa Paris Saint-Germainwakifurahia kutwaa kombe la klabu bingwa nchini Ufaransa (Coupe de France) baada ya kuifunga Monaco bao 1-0 mwaka 2010.. REUTERS/Benoit Tessier
Matangazo ya kibiashara

Cavani ambaye yuko likizo baada ya michuano ya kombe la dunia, na wachezaji wengine kutoka Ufaransa, Blaise Matuidi, Yohane Cabaye na Lucas Digne.

Wachezaji wengine kutoka mataifa ya kigeni ambao tayari wamejiunga na Paris SG ni Marco Verratti, Thiago Motta na Salvatore Sirigu ambao wote ni kutoka Italia.

Wachezaji wengine kama Thiago Silva, Maxwell na Davd Luis kutoka Brazil pamona na Ezequiel Lavezzi kutoka Argentina, watajiunga na kikosi cha klabu ya PSG mwanzoni mwa mwezi wa Ogasti.

PSG inajiandaa kucheza mechi ya kirafiki na Nice kwenye uwanja wa Béziers kusini mwa Ufaransa, kabla ya kujielekeza Hong Kong kuchuana na vilabu Kitchee ifikapo jumanne Juali 29.

Klabu hio ambayo ni klabu bingwa nchini Ufaransa itajielekeza baadae katika mji mkuu wa China Pekin, ambapo itachuana Ogasti 2 na klabu ya Guingamp.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.