Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Mandanda aachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kinachoelekea Brazil 2014

Benchi la ufundi la timu ya taifa ya Ufaransa hatimaye limethibitisha kipa wa klabu ya St Etienne, Stephane Ruffier kwenye kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 watakaoenda na timu hiyo nchini Brazil kushiriki fainali za kombe la dunia 2014.  

Mlinda mlango, Steve Mandanda ambaye ameachwa kwenye kikosi kamili cha timu ya taifa ya Ufaransa.
Mlinda mlango, Steve Mandanda ambaye ameachwa kwenye kikosi kamili cha timu ya taifa ya Ufaransa. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kujumuishwa kwenye kikosi cha Ufaransa cha wachezaji 23 wanaoenda nchini Brazil kumetokana na majeraha aliyoyapata mlinda mlango, Steve Mandanda baada ya kuumia shingo wakati akichezea timu yake ya Marseille kwenye mchezo wa mwisho wa kufunga pazia la ligi kuu ya Ufaransa.

Steve Mandanda.
Steve Mandanda. REUTERS/Kai Pfaffenbach

Ufaransa iko kwenye kundi E pamoja na timu ya taifa ya Ecuador, Honduras na Uswisi.

Timu hii inaundwa na walinda mlango, Hugo Lloris (Tottenham Hotspur), Stephane Ruffier (St Etienne), Mickael Landreau (Bastia).

Walinzi ni pamoja na, Mathieu Debuchy (Newcastle), Lucas Digne (Paris St-Germain) Patrice Evra (Manchester United), Laurent Koscielny, Bacary Sagna (both Arsenal), Eliaquim Mangala (Porto), Mamadou Sakho (Liverpool), Raphael Varane (Real Madrid).

Viungo wataongozwa na, Yohan Cabaye, Blaise Matuidi (both Paris St-Germain), Clement Grenier (Lyon), Rio Mavuba (Lille), Paul Pogba (Juventus), Moussa Sissoko (Newcastle), Mathieu Valbuena (Marseille).

Huku safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Karim Benzema (Real Madrid), Olivier Giroud (Arsenal), Antoine Griezmann (Real Sociedad), Loic Remy (Newastle, on loan from QPR), Franck Ribery (Bayern Munich).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.