Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Wasifu wa Timu ya Taifa ya Uholanzi

Imeshiriki mara 9, haijawahi kushinda taji hili, iko katika nafasi ya 15 kwenye viwango vya FIFA.Historia kwenye kombe la dunia la FIFA.Timu ya taifa ya Uholanzi inafahamika sana kama “The Orange”, Ikiwa chini ya kocha mkongwe Rinus Michels na benchi la ufundi lililokuwa na wachezaji kama Johan Cruyff, Johan Neeskens and Co walishinda na hadi kufika fainali mwaka 1974 na kupoteza mchezo wao kwa timu mwenyeji. Miaka minne baadae walishiriki tena na kufika fainali mwaka 1978 nchini Argentina lakini wakashindwa tena kwa mwenyeji wa michuano hiyo. Kwa mara ya tatu mfululizo timu ya taifa ya Uholanzi ilijikuta ikishindwa kutimiza ndoto za kutwaa taji hilo baada ya kufika fainali kwenye kombe la dunia la mwaka 2010 nchini Brazil na kufungwa kwa njia ya matuta na timu ya taifa ya Uhispania. 

Timu ya taifa ya Uholanzi
Timu ya taifa ya Uholanzi fifa.com
Matangazo ya kibiashara

Kundi ililopo.

Timu ya taifa ya Uholanzi iko kwenye kundi B kwenye michuano ya mwaka huu nchini Brazili ikijumuishwa pamoja na timu za Uhispania, Chile na Australia.

Wachezaji wakuangaliwa.

Uholanzi ni moja kati ya timu ambazo zinawachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa nchini Uingereza na Ujerumani, wachezaji kama Robin van Persie anayekipiga na klabu ya Manchester United ya Uingereza, Arjen Roben anayekipiga na klabu ya Bayern Munich ni miongoni mwa wachezaji wanaopewa nafasi ya kuisadia timu ya Uholanzi. Wengine ni pamoja na Jermaine Lens, rafael van der Vaart, Kevin Strootman na Daryl Janmaat.

Benchi la Ufundi.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uholanzi ni Louis Van Gaal.

Mafanikio pekee kwenye fainali za kombe la dunia la FIFA.

Ilikuwa mshindi wa pili kwenye fainali za kombe la dunia la FIFA mwaka 1974 nchini Ujerumani, mwaka 1978 nchini Argentina, mwaka 2010 nchini Afrika Kusini. Ilimaliza mshindi wa tatu kwenye michuano ya Olympic ya london mwaka 1908, vijana chini ya umri wa miaka 17 nchini Peru mwaka 2005 na kuwa mshindi wa tatu.

Wachezaji waliovuma.

Ni pamoja na Johan Cruyff, Marco van Basten na Dennis Berhkamp.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.