Pata taarifa kuu
UEFA

Chelsea na Real Madrid zafuzu nusu fainali michuano ya UEFA

Klabu ya soka ya Chelsea kutoka nchini Uingereza imefuzu katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya  UEFA baada ya kuishinda  Paris Saint Germain ya Ufaransa mabao 2 kwa 0 Jumanne  usiku katika uwanja wa Stamford Bridge.

Demba Ba mshambulizi wa klabu ya Chelsea
Demba Ba mshambulizi wa klabu ya Chelsea Reuters
Matangazo ya kibiashara

Huu ulikuwa ni mchuano wa marudiano baina ya vlabu hivyo viwili na ushindi huo ulikuwa muhimu sana kwa vijana wa kocha Jose Mourinho waliopoteza mchuano wa kwanza kwa kufungwa mabao 3 kwa 1 jijini Paris, na hivyo wamefuzu kutokana na bao la ugenini walilolipata jijini Paris baada ya kutoka kwa jumla ya mabao 3 kwa 3.

Bao la mshambulizi wa Kimataifa wa Senegal Demba Ba katika dakika ya 87 ya mchuano huo liliinua Chelsea baada ya bao la ufunguzi lililotiwa kimyani na mshambulizi mwingine Andre Schuerrle.

Kwa muda mrefu  Ba amekuwa hapati nafasi katika kikosi cha kwanza cha Chelsea na huenda bao la jana likamfanya Mourrihno kubadilisha mtazamo wake na kumpa nafasi ya mara kwa mara katika kikosi cha The Blues.

Mourinno ameongeza kuwa vijana wake wako tayari kumenyana na klabu yoyote katika hatua ya nusu fainali, hata kama ni Real Madrid klabu yake ya zamani.

Mbali na Chelsea, licha ya kufungwa na Borrusia Dortmund ya Ujerumani mabao 2 kwa 0, Real Madrid ya Uhispania pia wamefuzu kwa jumla ya mabao 3 kwa 2 kutokana na ushndi wa mabao 3 kwa 0 waliopata katika mchuano wa kwanza walipokuwa nyumbani.

Leo katika michuano mingine ya robo fainali, Atletico Madrid na Barcelona zote kutoka Uhisapia zitamenyana usiku,na katika  mchuano wa kwanza timu zote zilitoka sare ya bao 1 kwa 1.

Bayern Munich wa Ujerumani ambao pia ni mabingwa watetezi wa taji hili watakuwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Allianze Arena kuwakaribisha Manchester United ya Uingereza katika mchuano wa kukata na shoka.

Vlabu hivi viwili pia zilitoka sare ya bao 1 kwa 1 katika mchuano wa kwanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.