Pata taarifa kuu
Soka

Chelsea yairarua Tottenham 4-0 ligi kuu Uingereza

Magoli ya haraka yaliyofungwa na Samuel Eto'o na Eden Hazard yameing'arisha timu ya Chelsea jana Jumamosi kwenye mchezo wa kuwania taji la ligi kuu ya Uingereza. 

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho rfi
Matangazo ya kibiashara

Eto'o aliinynayua Chelsea katika dakika ya 56 na kisha Hazard akagongelea msumari wa moto kwenye kidonda cha Tottenham dakika nne baadaye baada ya Younes Kaboul kutolewa nje baada ya kumchezea vibaya Eto'o naye Demba Ba aliongeza baraka kwa Chelsea baadaye.

Chelsea kwa sasa inaongoza mbele ya Liverpool na Arsenal kwa alama saba, lakini timu zote mbili bado zina mchezo mmoja mkononi, Manchester City inayoshika nafasi ya nne ikiwa na alama 9 nyuma imesaliwa na michezo mitatu mkononi.

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho ameendelea kuishusha chini timu yake akisema kuwa anatamani angekuwa na nafasi ya Man City ambao wana michezo mitatu mkononi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.