Pata taarifa kuu
Soka Afrika

Yanga vs Al Ahly hapatoshi leo Dar es Salaam Tanzania

Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Dar es salaam Yanga Afrikans leo Jumamosi watashuka dimbani kumenyana na timu ya Aly Ahly ya nchini Misri katika mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza wa michuano ya klabu bingwa barani afrika katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam. 

Kikosi cha timu ya Yanga ya Tanzania
Kikosi cha timu ya Yanga ya Tanzania rfi
Matangazo ya kibiashara

Wachezaji watano wa timu ya soka ya Yanga waliokuwa kwenye kikosi cha Taifa (Taifa Stars), wameondolewa kwa ajili ya kuipa nafasi klabu hiyo ijiandae kikamilifu katika mechi yao ya marudiano ya raundi ya kwanza ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.


Nyota hao walioondolewa na hawataenda Windhoek kuwavaa Namibia (Brave Warriors) ni pamoja na kipa, Deogratius Munishi 'Dida', viungo, Athumani Iddi 'Chuji', David Luhende, Frank Domayo na winga, Mrisho Ngasa.



Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi, alisema pia wanatarajia kukiandikia barua Shirikisho la Soka la Uganda (Fufa) ili kuwaombea ruhusa, washambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi na Hamisi Kiiza, wasiende kwenye kikosi cha timu yao ya Taifa (Uganda Cranes) lengo likiwa ni kuifanya Yanga isipoteze nyota wake katika maandalizi wanayofanya.


Malinzi alisema wamefanya hivyo ili kuifanya Yanga inayokabiliwa na mechi ngumu iweze kushinda na kusonga mbele katika mashindano hayo ya Afrika.


Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.