Pata taarifa kuu
SOKA-UINGEREZA

Arsenal yafuzu kuingia raundi ya nne michuano ya ligi kuu nchini Uingereza

Klabu ya soka ya Arsenal imefanikiwa kutinga katika raundi ya nne ya kombe la ligi kuu ya Uingereza FA baada ya kuifunga Tottenham Hotspurs mabao 2-0 kwenye mtanange uliopigwa siku ya jumamosi katika dimba la Emirates.

Matangazo ya kibiashara

Bao la kwanza la Arsenal lilipachikwa na Santi Carzola, wakati bao la pili lilipachikwa na Tomas Rosicky katika nusu ya pili ya mtanange huo.

Hata hivyo mechi hiyo ilimalizika Arsenal ikiwa na wachezaji 10 pekee baada ya Theo Walcott kuumia goti katika dakika 10 za mwisho lakini Arsenal ilishindwa kuingiza mchezaji mwingine kwani walikuwa wameshabadili wachezaji watatu.

Arsenal imeendelea kujichimbia kileleni mwa ligi hiyo ikiwa na pointi 45, Manchester City iko katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 44, Chelsea ni ya tatu ikiwa na pointi 43 mbele ya Liverpool yenye pointi 39.

Mechi za raundi ya tatu zinazotarajiwa kupigwa hii leo ni baina ya West Ham na Nottingham Forest, Sunderland na Carlisle, Chelsea na Derby, Liverpool na Oldham, Port Vale na Plymouth wakati Manchester United watakuwa na kibarua dhidi ya Swansea.

Raundi ya nne ya michuano hiyo itaanza kupigwa kuanzia jumamosi ya tarehe 25 ya mwezi huu na fainali itakuwa ni mwezi Mei mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.