Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Arsenal yaongoza nafasi ya juu baada ya kuiyangusha West Ham

Theo Walcott aliifungia Arsenal mabao mawili huku Lukas Podolski akifunga la tatu katika mchuano wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya West Ham Hapo jana na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1. Ushindi huo wa Arsenal umewarudisha katika uongozi wa ligi kwa alama 39 alama moja juu ya Manchester City ambao wana alama 38 baada ya kupata ushindi dhidi ya Liverpool wa mabao 2-1.Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema ushindi wa jana wa Arsenal ulikuwa wa kuridhisha sana. 

Matangazo ya kibiashara

Wakati huohuo timu ya Manchester City, imeifunga imu ya Liverpool 2-1. Manchester City imepanda katika nafasi ya pili na kuruhusu Arsenal, mshindi wa West Ham kwa magoli 3-1 kuwa kiongozi wa juu baada ya siku ya 18 ya michuano hiyo ya Ligi ya Uingereza.

Katika michuano hiyo iliyofanyika katika muktadha wa “Boxing Day” kati ya timu mbili zinazovutia zaidi kwaa sasa, Manchester City wamemnyamazisha Suarez, mfungaji wa mabao 10 katika mechi nne .

Wakianza mechi hiyo kwa matatizo na hasa baada ya Coutinho kuliona lango la manchester, mashetani wekundu haraka wamejibu kwa mabao mawili ya Kompany na Negredo , ambaye ametumia nafasi ya kosa alilolifanya kipa wa mashetani hao.

Baada ya ushindi huo wa tano mfululizo katika mashindano mchanganyiko na kushinda mara 9 wakichezea nyumbani, wachezaji hao wa Pellegrini wanaendelea kupanda katika kuongoza na sasa wanashika nafasi ya pili.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.