Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Wachezaji wa timu tatu za Uingereza wasifiwa na Kocha wa timu ya Taifa ya nchi hio

Kocha wa England Roy Hodgson amesema amefurahishwa na hari ya sasa ya baadhi ya wachezaji wake, akibaini kwamba anataka kuwaweka kando ili awatumie wakati wa michuano ya Kombe la Dunia itakayochezwa nchini Brazil . Winga wa Tottenham Andros Townsend, mchezaji wa katikati wa West Ham, Ravel Morrison na mfungaji wa West Bromwich Albion, Saido Berahino , wameonyesha ubingwa wao katika michuano ya Ligi Kuu ya msimu huu.

Matangazo ya kibiashara

Roy Hodgson amebaini kwamba wachezaji hao watashirikishwa katika mechi ya kirafiki dhidi ya Denmark itakayochezwa mwezi machi kwenye uwanja wa Wembley.

"Hivi sasa, nimeona wengi wa wachezaji wetu na wale watakaojiunga na timu ya taifa wakicheza vizuri".

"Mimi ninasikitika kuona hatujaimarisha vilivyo hari ya wachezaji hawa, amesema Roy Hodgson kwenye Sky televisheni Sports News".

Hodgson amesema mechi zitakazochezwa ni za kuvutia, huku akibaini kwamba kuna timu nyingi wakati huu, ambazo zinawachezesha wachezaji wa Uingereza, akifahamisha kwamba amekua akiona mabadiliko kwa timu hizo .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.