Pata taarifa kuu
`UINGEREZA

Manchester City yaapa kuiangusha Liverpool kwenye nafasi ya kwanza

Katika michuano ya ligi ya Uingereza, Liverpool ambayo imesogea kwa shida kwenye nafasi ya kwanza, iko njiani ikijielekeza nyumbani kwa timu ya Manchester City ambayo ndoto yake ni kushikilia nafasi hio ya kwanza.Timu hizo mbili bingwa zinashindana alama moja pekee, licha ya kua Liverpool inachukua nafasi ya kwanza, huku Manchester City ikishikilia nafasi ya tatu.

Matangazo ya kibiashara

Arsenal ambayo inaishinda mabao Manchester City, inachukua nafasi ya pili.

Liverpool, kwa sasa imeshafunga mabao 17, huku mabao 10 yakiwa yalipachikwa wavuni na Suarez, huku Manchester City ikwa ina mabao 16 iliyoigingiza wavuni.

Manchester City ikibahatika kuifunga Liverpool, itakua imechukua nafasi ya kwanza.

Manchester City, ambayo ilifunga michuano 14 kati ya 17 katika hali ya kushangaza, imeapa kufanya vizuri nyumbani, kwa kumfunga mtani waake wa jadi Liverpool.

Nasri, Silva, Navas, Negredo aidha Dezko ni wachezaji tumaini wa Manchester City ambao muda wowote wataweza kuliona lango la Liverpool.

Liverpool haina wachezaji, ambao ni tishio kwa Manchester City, inamtegemea tu Suarez ambae ni kiungo tisha kwa Manchester City.

City ambayo inahesabu mabao 8 ambayo imeshaingizwa wavuni, itawakosa katika mchuno wake na Liverpool Zabalata na Richads.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.