Pata taarifa kuu
SOKA

Didier Drogba na Emmanuel Eboue kuchukuliwa hatua za kinidhamu baada ya kuvaa jezi zenye ujumbe wa kumuenzi Mandela

Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka nchini Uturuki TFF imewaita wachezaji wa Cote d'Ivoire wanaoichezea klabu ya Galatasaray, Didier Drogba na Emmanuel Eboue kufuatia kitendo cha kuvaa jezi zenye ujumbe wa kumuenzi kiongozi wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela aliyefariki dunia juma lililopita jijini Johannesburg.

http://babajidesalu.wordpress.com/
Matangazo ya kibiashara

TFF imesema wachezaji hao wameitwa na kamati ya nidhamu baada ya kuvaa jezi zenye kauli na ujumbe wa kisiasa tofauti na sheria za soka nchini humo.

Baada ya kutamatika kwa mechi baina ya Galatasaray na SB Elagizspor katika ligi ya Uturuki siku ya ijumaa, wachezaji hao walitoa fulana zao na kubaki na jezi za ndani zilizokuwa na maandishi yanayomaanisha “Asante Madiba” aliyovaa Drogba na jezi ya Eboue ilikuwa na ujumbe unaomaanisha “Pumzika kwa amani Mandela”

Hivi karibuni wachezaji wengine wa Fethiyespor walishtakiwa kwa kuvaa jezi zenye ujumbe wa kisiasa.

Drogba ambaye anatarajiwa kukiongoza kikosi cha Taifa lake wakati wa michuano ya kombe la dunia mwaka ujao nchini Brazil ameandika katika ukurasa wake wa facebook kuwa anataka kutuma salamu za rambirambi kwa familia ya Mandela, wapendwa wake na kwa watu wote wa Afrika Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.